Rebecca Muna
Dar es Salaam, Tanzania
Mimi ni Rebecca Muna, msanii wa mashairi na mtangazaji mwenye dhamira ya kutumia sanaa kuelimisha, kuhamasisha na kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Kupitia mashairi yangu, nimekuwa nikigusa maisha halisi ya vijana, changamoto za kijamii pamoja na umuhimu wa kujitambua na kuishi kwa kusudi. Ni mshindi wa Tanzania Emerging Youth Awards 2022 kama Young Artist of the Year – Female kupitia kipaji cha mashairi, pamoja na mshindi wa Youth in Business Awards 2025 kama Best Poet. Tuzo hizi zimekuwa uthibitisho wa mchango wangu katika kukuza sanaa yenye ujumbe wa kujenga jamii. Ninaamini kuwa maneno yana nguvu ya kuponya, kuhamasisha na kubadilisha maisha, hivyo ninaendelea kutumia kipaji changu kama sauti ya matumaini na mwanga kwa jamii.
Audio
3 tracksKijana Wa Thamani
Binti Mjamzito
Ndoa Ni Pingu Yangu