Nivard Mwageni
Dar es Salaam, Tanzania
Nivard Silvester Mwageni ni mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam katika Kituo cha Taaluma za Mawasiliano (Centre for Communication Studies) tangu 2022. Alianza kutunga na kughani mashairi tangu akiwa mwanafunzi ngazi ya sekondari ambako aliaminiwa kutunga mashairi kwenye matukio ya shule. Alipojiunga na elimu ya juu ndipo kipaji kilizidi kujidhihirisha baada ya kushiriki kuandaa kazi mbalimbali za ushairi za mazoezi ya darasani ya kozi za ushairi na matukio mbalimbali. Alipoajiriwa kwa mara ya kwanza kama mwalimu wa sekondari (2013) alipewa majukumu ya kusimamia masuala yote yahusuyo uimbaji ikiwemo na ushairi. Kwa sasa akiwa kama mhadhiri amekuwa anatunga mashairi yanayochapishwa kwenye majarida na magazeti kama vile jarida la UDASA na jarida la Kituo cha Taaluma za Mawasiliano. Amekuwa pia akishiriki matukio kwa kutunga na kughani mashairi kwenye majukwaa kama Poetry255.
Audio
3 tracksUgali Na Matembele
Kisasi Anaishi Wapi?
Siri Ya Kaburi