Nipaeli Mtana
Dar es Salaam, Tanzania
Nipaeli Amosi Mtana ni mwanzilishi na mkurugenzi wa Ubunifu wa Nipa Foundation, shirika linalotumia sanaa kama chombo cha kuwawezesha watu wenye ulemavu na kukuza ushiriki wao katika jamii. Ni msanii wa taaluma mbalimbali, ikiwemo ngoma ya kisasa ya watumiaji wa viti mwendo, ushairi wa maonesho, muziki, na usimamizi wa sanaa. Akiwa mtetezi wa haki za watu wenye ulemavu, Nipaeli ameongoza na kuratibu miradi mbalimbali ya ubunifu na ujumuishi inayolenga kujenga uwezo wa vijana na wanawake wenye ulemavu kupitia sanaa, ujasiriamali, na maendeleo ya jamii. Pia ameshiriki katika programu na mafunzo ya kitaifa na kimataifa yanayohusu usimamizi wa sanaa, ucuration, na uongozi. Kupitia kazi yake, anaamini kuwa sanaa ni daraja la kuondoa unyanyapaa, kubadili mitazamo, na kujenga jamii inayotoa fursa sawa kwa wote. Dhamira yake ni kuendelea kuunda nafasi salama na jumuishi ambapo watu wenye ulemavu wanaweza kuonyesha vipaji vyao, kusimulia hadithi zao, na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Audio
2 tracksMwanakwetu
Usawa