Moza Abdallah
Kaskazini, Unguja
Mimi ni Moza Abdalla Mohammed, mzaliwa wa Pemba, Tanzania. Nina miaka 21. Nasomea Counseling Psychology, taaluma iliyonipa uelewa mpana kuhusu maisha ya binadamu na umuhimu wa kuwasaidia wengine. Nimezaliwa na kipaji cha uandishi. Tangu nilipogundua uwezo wangu wa kuandika, nimekuwa nikiamini kuwa kalamu ni zawadi niliyopewa ili kuelimisha, kuhamasisha na kugusa maisha ya watu. Kwa sasa ndiyo kwanza ninaanza safari yangu ya uandishi, nikiwa na ndoto kubwa ya kuwa mwandishi wa vitabu vinavyoacha alama katika jamii na kugusa mioyo ya wasomaji. Ninaamini kuwa kila neno lina nguvu, kila simulizi lina ujumbe, na kila kitabu kinaweza kubadili maisha ya mtu. Hivyo, nitaendelea kuandika kwa bidii, ubunifu na uaminifu ili kutimiza ndoto yangu na kutoa mchango chanya kwa jamii kupitia kalamu yangu. Kaulimbiu yangu ni: "Napiga kalamu na historia inaandika."
Audio
3 tracksRafiki Wa Kweli
Athari Za Mitandao Ya Kijamii
Asili Ya Zanzibar