WahengaWapya
HA

Hamida Ahmed

Mjini Magharib, Unguja

MelodicCommunity#Mithali#Jamii#Nafsi#Parable#Society#Self#Kiswahili Poetry

Naitwa Hamida Ahmed Ali Ni mshairi niliyezaliwa katika Hospitali ya Sebleni wilaya ya magharib A Unguja tarehe 10/2/1986. Mwaka 1995 hadi mwaka 2001nilipata elimu ya msingi katika Skuli ya Kajificheni iliyopo wilaya ya mjini, mkoa wa mjini Magharibi Unguja.Mwaka 2002 hadi mwaka 2006 nilijiunga na masomo ya Sekondari katika Skuli ya Forodhani mjini Zanzibar. Mwaka 2010 nilipata elimu ya cheti katika chuo cha habari. Na nilihitimu elimu ya kiislamu katika chuo kilichopo Gulioni Zanzibar. Kwa sasa mimi ni Mkaazi wa Kwarara wilaya ya Magharibi B Zanzibar na mtunzi wa mashairi na hadithi Napenda zaidi kusoma vitabu vyamashairi na riwaya ,nilianza kutunga mashairi mwaka 2008 nilipata mafunzo ya utunzi kwa Mwalimu Abasi Mdungi na Mwalimu Ali Mwalimu Rashid. Mashairi yangu yanasomwa Zbc radio na kuchapishwa katika gazeti la Serikali, Zanzibar Leo.

Audio

3 tracks

Jiko La Kuni

0:00 / 2:28

Njoo

0:00 / 1:15

Wanawake Na Watoto

0:00 / 1:41