WahengaWapya
Portrait of Getrud TomGT

Getrud Tom

Arusha, Tanzania

Spoken WordIdentity#Self#Values#Love#Growth#Relationships#Nafsi#Familia#Upendo#Mahusiano#English Poetry

Naitwa Getrud Thomas Mushi, maarufu kwa jina la kisanii Getrud Tom. Safari yangu ya uandishi ilianza nikiwa mwanafunzi wa shule ya sekondari, nilipovutiwa na somo la Literature, jambo lililonisukuma kuanza kuandika mashairi. Tangu wakati huo, nimeendelea kukuza kipaji changu kupitia uandishi wa mashairi mafupi (micro poems) na mashairi ya kisasa, ambapo kazi zangu nyingi huandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Katika safari yangu ya kisanaa, nilijiunga na Arusha Poetry Club, ambako nilipata fursa ya kujifunza kutoka kwa washairi na wasanii wengine, kukuza uwezo wangu wa kisanaa na kuonesha kipaji changu kwa hadhira mbalimbali. Mwaka 2017, niliwasilisha shairi langu la kwanza lililorekodiwa, “Soulmate,” kupitia Poetry Shule – Home of Literary Work, hatua iliyoashiria mwanzo wa safari yangu ya kitaaluma katika ulimwengu wa mashairi. Mbali na uandishi, mimi ni spoken word poet, ninayetumia jukwaa kuwasilisha mashairi yenye kugusa hisia, kuibua tafakari na kuhamasisha jamii. Ninaamini kuwa sanaa ya neno ina uwezo wa kuunganisha watu, kuanzisha mazungumzo yenye maana na kuleta mabadiliko chanya. Kupitia kalamu na jukwaa, ninaendelea kutumia mashairi kama daraja la kuunganisha hisia, fikra na maisha. Mitandao ya Kijamii * TikTok@GetrudTom * Instagram: @GetrudTom

Audio

3 tracks

Mama

0:00 / 1:06

I Love Myself

0:00 / 1:04

Blue Mornings

0:00 / 1:11